The House of Favourite Newspapers

Makonda amtembelea kijana mwenye uvimbe usoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akiwa na Hamza Ashiraf.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amemtembelea kijana aitwaye Hamza Ashiraf ambaye hivi karibuni alimsaidia kwa kumsafirisha kutoka nyumbani kwao Bukoba na kumleta jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi juu ya uvimbe wake kwenye paji la uso.

 

Siku chache zilizopita kijana Ashiraf akiwa kwao Bukoba, alijitokeza hadharani kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu ya tatizo lake la uvimbe uliojitokeza kwenye eneo la uso wake.

 

Lakini kwa kudra za Mwenyenzi Mungu, Makonda alijitoa kumsaidia na mara moja akamfanyia utaratibu wa ndege ya kumfikisha jijini Dar es Salama na mara moja akaelekeza apelekwe katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi,  jambo ambalo tayari limeshafanyika na kwamba siku chache zijazo atafanyiwa upasuaji mkubwa ambao utapelekea sehemu kubwa ya uvimbe huo kutoka.

 

Taarifa kutoka kwa Daktari  Bingwa wa Upasuaji wa Macho na masikio, Edwin Lyombo, amesema, wakati Ashiraf anatolewa Bukoba tayari alikuwa ameshaanza kufanyiwa matibabu lakini hayakuwa mazuri.

“Nitoe shukurani nyingi kwa Mheshimiwa Makonda kwa moyo wake wa kujitolea kama huu, kwani endapo watu wengi aaidi watapatikana kujitolea hapa nchini kusaidia watu wenye matatizo makubwa kama haya,  basi uwezekano wa kupunguza maradhi makubwa kama haya utaleta tija,” alisema Lyombo.

 

Ashiraf  ameendelea kutoa shukurani zake kwa Makonda kwa kumwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Niendelee kutoa shukurani zangu kwa Mheshimiwa Makonda kwa kuendelea kutoa mahitaji yote hadi muda huu, na kwamba niwaambie tu Watanzania kuwa wasiwe na hofu na mimi kwani nipo kwenye mikono salama kabisa,” alisema Ashiraf.

Comments are closed.