The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Aongeza Muda wa Kupiga muziki Usiku (Picha + Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiongea na wananchi wa jiji la Dar es Salaam katika Uwanja wa Magunia Tandale jijini.

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda leo ametangaza kuondoa muda wa kikomo kwa wasanii kupiga mziki kwenye matamasha hadi saa sita usiku na sasa amewaongezea muda hadi Saa nane usiku kwa siku za wikiendi pekee.

Umati wa wananchi wa Tandale ukiwa katika Uwanja wa Magunia.

Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe na wasanii nchini ambao kilio chao kilikuwa kuongezewa muda wa kufanya matamasha ili waweze kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha kuendana na kaulimbiu ya Rais wao Mpendwa Dkt. John Magufuli inayowataka watu kufanya kazi.

Hii pia ni matokeo ya kuimarika kwa ulinzi na usalama wa jiji hilo la kibiashara ambapo lengo la RC Makonda ni kuona siku moja watu wanafanya shughuli za kibiashara kwa Saa 24.

Shangwe nyingine Makonda baada ya kupewa nafasi na kueleza jinsi alivyokuwa mlezi wa WCB na kumtaka Diamond aoe kabla mwaka haujaisha. “Leo hii Diamond akimtaka hata mwanamke wa aina gani atampata kwa sababu ana kipaji.

Mstahiki Meya wa Kindondoni, Benjamini Sitta.

Kuna mstahiki Meya hapa (Benjamini Sitta) nimemwambia mwaka huu ukiisha asipooa namfunga, kuna mwingine naye anaitwa Majizzo yeye juzi kaniwahi kamvisha pete Lulu (Elizabeth Michael).

 

“Lakini nilikuwa najiuliza huyu naye (Diamond) tumtie ndani au tufanyeje? Lakini nimegundua kwa kazi aliyonayo, Diamond nampa miaka acha kwanza aendelee kuwa sukari ya mioyo ya watu, namtaka baadaye awe zaidi ya kina 50 Cent na Jay Z si mnaona hata Jay Z alifanya muziki akaweka mambo yake.

William Malecela, maarufu kama Lemutuz Nation au “King of All Bongo Social Networks” akiongea jambo.

PICHA: RICHARD BUKOS, GPL

Comments are closed.