The House of Favourite Newspapers

MAKONDA, AONGOZA WASANII KUTEMBELEA MRADI WA SGR (PICHA +VIDEO)

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo amewaongoza wasanii na waandishi wa habari kwa ajili ya kutembelea na kujionea namna shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme, Standard Gauge Railway (SGR),  kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro unavyoendelea, ambapo treni hiyo imeondoka leo na wasanii na wanahabari wa vyombo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC),  Masanja Kadogosa, wakati alipowasili katika ziara ya kuwaongoza wasanii kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ijulikanayo kama Standard Gauge Railway (SGR).
…Akizungumza jambo kabla ya kukagua mradi huo.
…Akitembezwa eneo la mradi akiwa amefuatana na wasanii.
…Akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Kagodosa.
Ujenzi ukiendelea chini ya  kampuni ya Yapi Merkezi.
Meneja wa kundi la wasanii la Wafafi Classic Baby (WCB) Babu Tale (wa tatu kushoto) na promota wa ngumi, Kaike (T-shirt  nyeupe) ni miongoni mwa watu waliojiambatana na wasanii wengine katika ziara hiyo
Wasanii Peter Msechu (kushoto) na Mrisho Mpoto (kulia) wakiwa katika ziara hiyo.
Baadhi ya wasanii kabla ya kupanda treni na kuanza safari ya kwenda Morogoro.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.