The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Awataka Wakuu Wa Wilaya Kutenga Siku Tatu Za Kusikiliza Kero Za Wananchi Kwenye Maeneo Yao

0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Missaile Albano Musa kuwaandikia barua rasmi ya kuwataka Wakuu wa Wilaya Mkoani humo kutenga siku tatu za kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Mhe. Makonda ameyasema haya Mei 10, 2024 alipokuwa akiendelea na kliniki ya Haki siku ya tatu mfukulizo ambapo Leo amewasililiza Wananchi ana kwa ana na kutatua Changamoto zao

“Tukifika kwenye ziara Wilayani kwako, Kwa mfano tukiwa Karatu Mkuu wa Wilaya atuambie huyu tulimsikiliza na kutatua kero yake Kwa namna Fulani na tumekwama eneo hili Mkuu wa Mkoa tusaidie”Amesema.

Amesema heshima ya Jiji la Arusha ipo maeneo ya mijini tu, lakini ukiingia ndani Wilayani ni kama vile hakuna watu wa Mipango miji, hivyo amewataka watendaji wote kuhakikisha kuwa wanasimamia ipasavyo Sekta ya Ardhi.

MTOTO ALAWITIWA ANAJISAIDIA DAMU- MAMA AAMBIWA HANA NYOTA ya KUTEMBEA na POLISI NDIO MAANA HASAIDIWI

Leave A Reply