RC Makonda Awatuliza Mashabiki, MO Dewji Kujiuzulu Simba SC

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Simba SC, usiku wa kuamkia leo ametumia ukurasa wake wa insta kuwaomba mashabiki wwa Simba watulie, kuhusiana na taarifa ya twitter ya mwenyeki wao wa bodi MO Dewji kutangaza kujiuzulu nafasi yake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, kutokana na Simba kufungwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Matokea ya Mpira huleta furaha na huzuni kwa wanaofungwa. Natoa pole Kwa team yangu ya Simba pamoja na Mashabiki wote na wanaoitakia mema SIMBA. Sina uhakika na kinachoendelea kwenye Ac ya MO kama ni @moodewji mwenyewe ameandika. Nawaomba wanasimba tutulie tutapata ukweli muda si mrefu. Tusisahau kuwa Wapo watu pia wabaya hutumia mwanya huu kuvuruga Amani na utulivu wa Team zetu. Simba nguvu moja.” alisema RC Makonda

Toa comment