The House of Favourite Newspapers

RC MAKONDA: “DUDU BAYA TULIA KWANZA” – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya‘ kutulia badala ya kutaja majina ya baadhi ya wanahabari wa kiume mitandaoni na kuwatuhumu kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

 

Akizungumza na wanahabari wakati akikabishi magari kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa, Novemba 2, 2018 Makonda amesema msanii huyo anatakiwa kufuata utaratibu uliyowekwa wa kutuma majina kwa njia ya simu kwenye namba iliyowekwa badala ya kutaja hadharani.

 

“Nimesikia kuna watu wanatajwa, mtu anarekodi huku anataja, nilipoona mara ya kwanza nikasema tusingependa kuleta taharuki, hili zoezi tunatakiwa kulifanya kwa umakini sana, ikabidi nitafute namba yake ilki nimuombe kwamba ’embu tulia kwanza, taarifa kama unazo tutumie kwa meseji’.

 

“Nilichostuka ni kwamba jamaa (Dudu Baya) anasema wakipimwa wakabainika siyo mashoga, yupo tayari kufungwa jela, jamaa ana uhakika, ameniacha hoi, hawa wote amejuaje? Hii ni kama wachawi, wanaroga usiku lakini watu wanawajua kwamba flani ni mchawi,” amesema Makonda.

 

Makonda amewaomba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa watulivu na kuendelea kutoa taarifa kupitia namba za simu zilizotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama vitafanyia kazi huku akiwataka pia kukemea vitendo hivyo vovu.

 

VIDEO: MSIKIE MAKONDA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.