RC Makonda: Kuhakiki Taarifa za Mpiga Kura Dar Mwisho Leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda leo Mei 3, 2020 amewataka wakazi wa Dar es Salaam ambao bado hawajahakiki taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, kufanya hivyo bila kuchelewa kwakuwa mzunguko wa pili wa zoezi hilo kwa jiji la Dar es Salaam unamalizika leo.

“Nendeni mkahakiki taarifa zenu, ili baadae msije kujilaumu kwa kukosa haki ya kupiga kura kwakuwa tu taarifa zenu hazijahakikiwa, tahadhari zote za kujikinga na corona zimechukuliwa kwenye vituo ikiwemo kuweka maji tiririka na sabuni na Watu kutosogeleana” alisema RC Makonda

Mzunguko wa pili wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura unafanyika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Iringa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Moro, Pwani na DSM na umeanzia May 02 hadi kesho May 04, 2020.


Toa comment