Video: RC Makonda Kutumia Bilioni 2.5 Kujenga Ofisi za CCM Dar

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Makonda amesema atatumia Sh2.5 bilioni kujenga ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Temeke, Kigamboni, Ubungo, Ilala na Kinondoni.

 

Katika maelezo yake, Makonda amesema, “wanaohoji kwamba fedha za Serikali zinatumika kujenga ofisi ya chama, wahoji kuhusu ofisi 73 za walimu zilizojengwa katika shule hapa Dar es Salaam, wahoji kuhusu watoto wanaopewa matibabu ya moyo na hospitali ya Chanika wahoji fedha zake zinatoka wapi.”


Toa comment