The House of Favourite Newspapers

RC MAKONDA, MEYA MWITA, WATEMBELEA MSAMVU STAND – MORO

Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda, Meya wa Jiji, Isaya Mwita na Mkurugenzi wa Jiji, Spora Liyana na baadhi ya madiwani wa jiji hilo leo wametembelea katika Kituo cha Msamvu mjini Morogoro.

Akizungumza kituoni hapo, Meya wa Mji wa Morogoro, Pascal Kihanga amesema kituo hicho kilichogharimu bilion 12 kimeanza kazi mwaka 2016 na mpaka sasa kimshatoa ajira 176.

“Tumejenga kituo hiki kwa ubia na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), Rais Dkt. John Magufuli alipokizindua rasmi mwaka jana aliahidi kutusaudia fedha ili kukifanya kiwe mali ya Halmashauri kwa asilimia 100. Kupitia kituo hiki, tunakusanya mapato zaidi ya milion tatu kwa siku,” alisema Kihanga.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dar, Mwita mbali ya kuipongeza halmashauri hiyo kwa kuwa na kituo hicho bora na cha kisasa Afrika Mashariki, amesema ziara yao mkoani hapa ilikuwa na lengo la kujifunza imekuwa na tija kubwa.

 

“Sisi wa Dar, tunatarajia kujenga stendi kubwa mara nne zaidi ya hii pale Mbezi ambapo tumetenga Shilingi bilion 50, hivyo tumejifunza mengi na tutakapoanza ujenzi wetu haya tuliyoyapata hapa leo yatatusaidia kufanikisha kwa maenedeleo ya Watanzania wenzetu,” alisema Mwita.

Na Dunstan Shekidele Morogoro | Global Publishers.

EXCLUSIVE: Sapraizi ya AY na King Kikii ni Habari Nyingine

Comments are closed.