RC Makonda: Tulieni Polisi Wanafanyia Kazi Utekaji wa Mo Dewji

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiongea na wanahabari katika Hoteli ya  Colosseum, Oyster Bay jijini Dar es Salaam kuhusu kutekwa kwa mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji.  Kulia ni Msemaji wa  Klabu ya Simba,  Haji Manara.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa,  akiongea na wanahabari.

…Akisalimia viongozi eneo la tukio.

Viongozi mbalimbali wakiongea kuhusu tukio hilo.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba wakazi wa Dar es Salaam kutulia wakati huu kuhusu kutekwa mfanyabiashara na mwekezaji katika Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji) kwani jeshi la polisi tayari limeshaanza uchunguzi na limebaini watekaji ni Wazungu raia wa nchi za nje.  Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki kutoa taarifa za utekwaji  wa mtu huyo uliofanyika katika gym ya Hoteli ya Colosseum, Oyster Bay jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo, ili kurahisisha kazi ya polisi.

PICHA/HABARI: MUSA MATEJA | GPL

Loading...

Toa comment