The House of Favourite Newspapers

Rc Telack: Shinyanga Haina Mauaji ya Vikongwe

0

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amesema Mkoa wa Shinyanga hauna tena mauaji ya vikongwe kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na vyombo vya vya ulinzi na usalama zilizofanikisha kuyakamata makundi ya mapanga yaliyokuwa yanatekeleza mauaji hayo Mkoani Shinyanga.

 

Bi. Telack alisema hayo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha siku moja Aprili 11, na Shirika la Msichana Initiative na Championi wa kutokomeza ndoa za utotoni mkoani Shinyanga kilichowakutanisha baadhi ya wabunge ambao wanaunda kikundi hicho pamoja na wadau wengine waliokutana leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

 

Bi. Telack aliongeza kuwa kipindi cha nyuma vyombo vya habari kila kukicha vilikuwa vinaandika sana kuhusu mauaji ya mama wazee waliokuwa wanauawa kutokana na ramli chonganishi lakini sasa hali ni shwari na vyombo vya habari havitoi tena habari za mauaji hayo kwani hayapo tena.

 

Kuhusu mimba na ndoa za utotoni Bi. Telack alisema kuwa juhudi zilizofanyika ni pamoja na kukamata watoto wakiwa wanafungisha ndoa na juhudi hizo zilifanyika baada ya Mkoa huo kuwa na takwimu za juu kwani awali Mkoa wa Shinyanga uliongoza 59% ya ndoa za utotoni nchini.

Leave A Reply