The House of Favourite Newspapers

Real, Atletico Kutifuana April 8

KIPUTE cha wapinzani wa jadi wa jiji la Madrid kinachozikutanisha Real na Atletico kitapigwa Aprili 8, mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

 

Kulikuwa na wasiwasi kuwa mechi hiyo, huenda ikaahirishwa kutokana na ushiriki wa timu hizo kwenye michuano ya Ulaya.

 

Real Madrid na Atletico Madrid zimefuzu kwa robo fainali ya mashindano ya Ulaya. Real imo Ligi ya Mabingwa wakati Atletico iko kwenye Europa

Tarehe ya Aprili 8 itakuwa siku ya Jumapili, lakini wiki inayofuata kutakuwa na mechi za robo fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Europa.

 

Real Madrid iliwasiliana na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kuwataarifu juu ya suala hilo lakini wamehakikishiwa kuwa watapangiwa Jumatano ya wiki inayofuata ili kupata muda wa kutosha wa mapumziko.

Hata hivyo, Kamati ya La Liga bado haijapanga muda wa mechi hiyo kwani siku hiyo pia kutakuwepo mashindano ya marathon ya jiji la Madrid.

Comments are closed.