RECHO ATANGAZA KUWA SINGO NDANI YA 255 GLOBAL RADIO

Mwanamuziki Recho (wa pili kushoto) akiwa na watangazaji wa kipindi cha Bongo 255.

MREMBO kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’ amesema kwa sasa hana mpenzi, yupo singo.

Recho alisema hayo leo Septemba18, 2019 alipokuwa akipiga stori na +255 Global Radio ambapo pamoja na mambo mengine kuhusu muziki, alizungumzia pia masuala ya mahusiano.

“Nipo singo kwa sasa japo huko nyuma zilipita stori nyingi sijui Recho ameolewa Uarabuni wakati si kweli. Kule nilipata boyfriend lakini tulishaachana,” alisema Recho.

 

Mrembo huyo alisema kati ya vitu ambavyo vimemuumiza maishani ni skendo ya kutumia madawa ya kulevya ambayo kwa sasa hapendi kuizungumzia kwani inamuumiza.

 

“Ningependa tusiizungumzie sababu inaniumiza na haina ukweli,” alisema Recho.

Kuhusu ukimya wake kwenye gemu, Recho alisema aliamua tu kuusoma mchezo lakini sasa amerejea kitofauti.

“Ukimya wangu una vitu vingi, nimeingia studio, nina nyimbo nyingi sana ambazo bado hazijatoka hivyo mashabiki wajiandae kunipokea,” alisema Recho na kuutambulisha wimbo wake mpya uitwao Chocho.

Ili kuyapata mahojiano kamili, ingia www.globalradio.co.tz.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani


Loading...

Toa comment