Refa Asimamishwa Kazi kwa Kutumia Simu ya Shabaki Kukataa Goli
Mwamuzi wa Misri Mohamed Farouk amesimamishwa kazi kwa kutumia simu ya mtazamaji kukataa bao katika mechi ya ligi.
Al-Nasr walidhani walikuwa wamefunga bao la kusawazisha dakika za lala salama wakiwa ugenini kwa Suez katika mechi ya ligi ya daraja la pili Ijumaa iliyopita.
Hakuna mwamuzi msaidizi wa video (VAR) katika daraja la pili la Misri, lakini Farouk alitumia simu kutazama video ya marudio baada ya wenyeji kulalamika kuwa kuna mchezaji aliyeugusa mpira kwa mkono.
Farouk kisha alifanya uamuzi wa kulikataa bao hilo. Shirikisho la Soka la Misri lilisema katika taarifa yake kwamba Vitor Pereira, ambaye alichukua nafasi ya Mark Clattenburg kama mkuu wa Kamati ya Waamuzi wa Misri mapema mwezi huu, aliamua kuwasimamisha kazi waamuzi wote kwa “muda usiojulikana”.
“Kamati iliamua kuchunguza tukio wakati Mohamed Farouk, mwamuzi wa mechi hiyo alipotumia simu ya mkononi kukagua picha za matukio ya mechi hiyo,” FA ya Misri iliongeza.
Suez ilifunga bao la tatu muda mfupi baada ya bao lililokataliwa na kupelekea ushindi wa 3-1, zikiwa zimesalia dakika 15 za mapumziko.
Farouk aliondoka uwanjani chini ya ulinzi wa polisi, huku kukiwa na maandamano ya wachezaji na viongozi wa Al-Nasr, ambao wametishia kumchukulia hatua za kisheria mwamuzi huyo kwa kukiuka kanuni.