The House of Favourite Newspapers

Refa wa PSG Kuzichezesha Simba SC vs Vita

Noureddine El Jaafari raia wa Morocco

 

REFA wa mechi ya leo kati ya Simba dhidi ya AS Vita siyo wa kitoto kwani amewahi kuchezesha mechi ya PSG ya Ufaransa ambayo anaichezea nyota mkubwa wa dunia, Neymar.

 

Mwamuzi huyo Noureddine El Jaafari raia wa Morocco ya Mabingwa Afrika katika ya Simba na Vita ambayo itapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kikosi cha timu ya Simba SC.

Katika msimamo wa kundi hilo Simba wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na pointi sita huku Vita na Al Ahly wakiwa na pointi saba. Vinara ni JS Saoura wenye nane.

 

Rekodi za mwamuzi huyo ambaye ni mwepesi wa kugawa kadi akiwa amefanya hivyo mara 83 za njano na mbili nyekundu katika mechi 31, inaonyesha alishawahi kuwachezesha PSG dhidi ya Monaco katika mechi inayowahusisha mshindi wa Ligi ya Ufaransa ‘Ligue 1’ na Kombe la Ufaransa (Trophée des Champions) iliyopigwa mwaka 2017 katika Uwanja wa Grand de Tanger nchini Morocco.

 

Mechi hiyo ilimalizika kwa PSG kushinda kwa mabao 2-1. Mabao ya PSG yalifungwa na Dani Alves na Adrien Rabbiot huku lile la Monaco likifungwa na Djibril Sidibé.

 

Kwenye mechi hiyo Mmorocco huyo aliwapa kadi za njano mastaa Marco Verratti (PSG), Fabinho Tavares, Sidibe na Kamil Glik wa Monaco.

 

Fabinho kwa sasa yuko Liverpool. Katika mechi hiyo mwamuzi huyo alikuwa akipishana na nyota wenye majina makubwa kama Radamel Falcao, Kylian Mbappé, Edinson Cavani, Dani Alves, Thiago Silva, Thiago Motta na kocha wa sasa wa Arsenal, Unai Emery.

Comments are closed.