Rekodi Mpya Ya Davido Sambamba Na Kanye West, Drake, Beyonce (VIDEO)

 

STAA wa muziki wa Afro Pop kutoka Nigeria, Davido, usiku wa kuamkia Januari 28  mwaka huu ameweka historia ya msanii mdogo kutoka Afrika kwa kuujaza uwanja maarufu wa matamasha ya muziki wa The O2 Arena uliopo jijini London nchini Uingereza.

 

 

Katika shoo hiyo ya kipekee Davido amefanikiwa kuuza tiketi 20,000 ambazo ndiyo idadi ya watu wanaoingia kwenye uwanja huo.

 

 

Kwa matokeo hayo, Davido anakuwa ni msanii wa pili kutoka Afrika kujaza uwanja huo; hii ni baada ya Wizkid mwaka jana naye kufanya hivyo.

 

 

Mastaa wengine wa muziki wakubwa ambao walishawahi kujaza uwanja huo ni  Ed Sheeran, Beyoncé, Rihanna, Kanye West, Drake, Elton John Prince, Alicia Keys, Adele, Celine Dion, Britney Spears .

 

TAZAMA VIDEO YA SHOW YAKE

 

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment