The House of Favourite Newspapers

Rekodi Simba Haijawahi Kutokea Miaka Mitano

Kikosi cha timu ya Simba.

SIMBA ya Mfaransa, Pierre Lechantre imevunja rekodi yake ya misimu mitano ya mabao baada ya kufunga mabao 51, huku wakiwa wamesaliwa na michezo tisa ligi ya msimu huu kumalizika. Kinachotokea Simba kwa sasa hakikuwahi kutokea misimu mitano iliyopita, takwimu zinaonyesha kwamba hawakuwahi kufikisha idadi hiyo ya mabao licha ya kuwa na mastraika mbalimbali wa kigeni.

 

Simba katika misimu mitano haikuwa kufunga mabao zaidi ya 50 mpaka pale ligi inapomalizika huku wapinzani wao Yanga wakionekana kuwa vizuri kutokana na kufunga idadi kubwa ya mabao mara kwa mara ndani ya kipindi hicho.

 

Mpaka sasa Simba ambayo nahodha wake ni John Bocco na kipa namba moja ni Aishi Manula, imecheza jumla ya mechi 21 na kukusanya pointi 49 huku wakifunga mabao 51 na kinara wa kucheka na nyavu akitoka katika klabu hiyo ambaye ni Emmanuel Okwi mwenye mabao 16.

 

Msimu uliopita mpaka ligi inamalizika Simba ilifunga mabao 50 huku wapinzani wa Yanga wao wakifunga mabao 57 na Mnyama akamaliza nafasi ya pili kwenye msimamo. 2015/16, Simba baada ya kucheza michezo 30 ya ligi
ilifunga mabao 45 tu huku Yanga ikifunga mabao 70 msimu ule wa mwaka 2014/15, ligi inamalizika walifunga mabao 38 na Yanga wakafunga mabao 52.

 

Simba ikiwa chini ya Mcrotia mwenye mbwembwe nyingi, Zdravko Logarusic msimu wa 2013/14 ilifunga mabao 41 ikimaliza nafasi ya nne katika msimamo na Yanga wao wakifunga mabao 61 na msimu wa mwaka 2012/13, Simba ilifunga mabao 38 na Yanga wao wakafunga mabao 47.

STORI NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.