The House of Favourite Newspapers

REKODI YA KAGERE YAIFUNIKA YANGA

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda Meddie Kagere ndiye anayeubeba mchezo wa Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumapili ijayo.

 

Kagere ndiye anaingia kwenye mchezo huu akiwa na rekodi ya juu kuliko wachezaji wengine wote.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa na Simba akitokea klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya kwa dau la milioni 113 na kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye Ligi Kuu Bara kwenye usajili uliopita.

 

Kagere anaingia kwenye mchezo huo akiwa na mabao matano na amefunga kwenye michuano rasmi ambayo ni Ngao ya Jamii pamoja na Ligi Kuu kuanzia ametua Simba.

 

Katika Ligi Kuu amecheza jumla ya mechi tano na kuweza kufunga mabao manne katika mechi hizo ikiwa mchezo dhidi ya Mbao FC ambao walifungwa bao moja lakini nyota huyo alianzia benchi.

Hii ina maana kuwa kwenye kila mchezo ambao ameanza mchezaji huyo amefanikiwa kuifungia timu yake bao.

 

Mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, aliweza kufunga bao moja na hii inaonyesha wazi kuwa ana nafasi ya kufanya kweli dhidi ya Yanga kama ataanza.

 

Wachezaji wengine ambao wanasubiriwa kwa hamu kubwa kwenye mchezo huu ni Shiza Kichuya na Amissi Tambwe.

 

Kichuya tangu ameanza kucheza mechi za Simba na Yanga amefanikiwa kufunga mabao matatu, huku Tambwe ambaye ana mabao mawili kwenye ligi kwa sasa akiwa naye alishafunga mabao matatu.

NA MARTHA MBOMA,

Comments are closed.