The House of Favourite Newspapers

Rekodi ya Kamusoko iliyomtoa Haruna Niyonzima

1

02-Yanga+kiungoKiungo wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

Mohammed Mdose,

Dar es Salaam

MABAO ya kiungo wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko, yamekuwa na maajabu ya aina yake na kutengeneza kastori f’lani ka kuvutia katika mechi za ligi kuu tangu kuanza kwa msimu huu, Septemba 12, mwaka huu.

NIYONZIMANEW4Haruna Niyonzima.

Kamusoko ambaye alisajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea timu ya FC Platinum ya Ligi Kuu ya Zimbabwe, katika mabao 30 ya Yanga mpaka sasa, yeye amefunga manne.

Katika mabao hayo yote manne, Kamusoko ameyafunga kipindi cha pili na kinachofanya kuwa ni ya maajabu ni kuwa kila alipofunga hakuna tena mchezaji mwingine aliyeweza kufunga si wa timu yake tu bali hata wa timu pinzani.

 

Kamusoko alifunga bao lake la kwanza katika ligi kwenye ushindi wa mabao 4-1, walioupata mbele ya JKT Ruvu, ambapo alifunga katika dakika ya 87, huku mabao mengine yakifungwa dakika ya 30, 48, 50 na 62.

Mechi nyingine alizofunga ni dhidi ya African Sports, ambapo matokeo yalikuwa 1-0, alifunga dakika ya 90. Kwenye ushindi wa 4-0, mbele ya Stand United alifunga dakika ya 64 mengine yalifungwa dakika ya 18, 36 na 45 na mchezo wa mwisho ni dhidi ya Mbeya City, alifunga dakika ya 66 huku mengine yakifungwa dakika ya 37 na 65.

Kwa rekodi hii pengine ndiyo maana wameamua kuachana na Haruna Niyonzima kwani Kamusoko amekuwa na vitu adimu kuliko Niyonzima ambaye wamekuwa wakilia na nidhamu yake mbovu.

 

1 Comment
  1. Mchezaji Uchwara says

    “Fabregas” kama Fabregas.

Leave A Reply