The House of Favourite Newspapers

Rekodi ya Yanga Usiku… Simba kicheko

0

Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI|  Dar es Salaam

TIMU ya Yanga, kesho Jumamosi itashuka uwanjani kupambana na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa usiku katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru kutokana na Uwanja wa Taifa siku hiyo kuwa na shughuli nyingine.

Kutokana na hali hiyo, Yanga ikaiomba Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) mechi yao ichezwe Uwanja wa Taifa majira ya usiku baada ya kumalizika kwa shughuli hizo.

Hata hivyo, endapo mechi hiyo itapigwa usiku kama Yanga wana­vyotaka, itakuwa ni kicheko kwa Simba ambayo inachuana vilivyo na timu hiyo katika kuwania ub­ingwa wa ligi kuu msimu huu.

Kicheko hicho cha Simba kinatokana na rekodi za Yanga ilizonazo katika mechi zake ilizocheza usiku tangu kuanza kwa mwaka huu.

Katika uchunguzi uliofan­ywa na Championi Ijumaa, imegundulika kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, Yanga imecheza mechi nne tu usiku ambapo tatu kati ya hizo zilikuwa ni za michuano ya Kombe la Mapinduzi ilizocheza dhidi ya Simba, Azam pamoja na Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mechi nyingine ya nne ni ile ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyocheza ugenini dhidi ya MC Algers ya Algeria.

Katika mechi hizo zote, Yanga imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Jamhuri tena kwa idadi kubwa ya mabao ambayo ni 6-0, huku zilizobaki ikifungwa.

Ilipocheza na Azam katika michuano hiyo, ilifungwa kwa mabao 4-0 na baa­daye ikafungwa na Simba kwa penalti 4-2 baada ya dakika tisini kumalizika kwa suluhu.

Ilipopambana na MC Alger katika mechi yake ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika mchezo uliyofanyika nchini Algeria, Yanga ilifungwa mabao 4-0 na kutupwa nje ya michua­no hiyo.

Kutokana na uchun­guzi huo, mchezo wa kesho Jumamosi kama ukichezwa usiku unaweza kuwa na matokeo ma­baya kwa Yanga kwani rekodi zinaonyesha haina bahati ya kufanya vizuri kila inapocheza muda huo tofauti na inapocheza mchana.

Leave A Reply