visa

Rekodi yaibeba Simba CAF

ZIKIWA zimebaki takribani siku nne kabla ya Simba kuivaa UD do Songo kutoka Msumbuji, rekodi zinaonyesha kuwa Simba wana asilimia kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Jumapili ya wiki hii.

 

Tangu msimu uliopita, Simba katika michuano ya kimataifa haijapoteza mchezo wowote waliocheza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao ndiyo uwanja wanaoutumia kwa mechi zao za nyumbani.

Katika mchezo huo wa marudiano, Simba inaingia ikiwa na rekodi ya kushinda michezo mitano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kati ya sita iliyocheza hapo ambapo mmoja pekee ilitoka suluhu.

 

Michezo ambayo Simba ilibuka na ushindi walipocheza nyumbani kwenyeUwanja wa Taifa ni; Simba 4-1 Mbabane Swallows, Simba 3-1 Nkana, Simba 3-0 JS Saoura, Simba 1-0 Al Ahly na Simba 2-1 AS Vita Club.

Ule wa suluhu ni dhidi ya TP Mazembe. Simba na UD Songo zilipokutana Msumbiji, matokeo yalikuwa suluhu jambo ambalo linaipa nafasi kubwa Simba kusaka ushindi ili isonge hatua inayofuata.
Toa comment