The House of Favourite Newspapers

RICH MAVOKO AFUNGUKA MAISHA BAADA YA WCB

JUNI 2, 2016 ilikuwa siku ya kihistoria kwa staa wa Bongo Fleva, Richard Martin ‘Rich Mavoko’ baada ya kusaini kuitumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya staa wa muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Lakini baada ya miaka miwili upepo ulikuwa ndivyo sivyo baada ya Mavoko kutangaza kujiengua katika lebo hiyo na kufanya kazi kivyake. Katika sakata hilo la kujiengua, alipeleka malalamiko yake Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ya kutoridhishwa na mkataba aliokuwa amesaini na kuutumikia.

 

Ukiachilia mbali ishu hizo, tangu Mavoko aanze kufanya muziki kivyake tayari ana ‘singo’ kadhaa kwapani ikiwemo Ndegele, Hongera, Naogopa na Navumilia.

Over Ze Wekeend imemtafuta Mavoko na kufanya naye mahojiano ya ana kwa ana na kufunguka mikakati yake yote baada ya WCB, huyu hapa…

 

Over Ze Wekeend: Vipi Mavoko tangu ujiengue WCB, unaonaje upepo wa muziki wako?

Mavoko: Uko sawa tu na haujawahi kubadilika hata kidogo yaani kwa upande wangu naona uko freshi tu na maisha yanaendelea.

Over Ze Weekend: Ngoma ambayo umetoa ya Naogopa imepokelewaje na mashabiki wako maana ni muda kidogo ulikuwa kimya?

Mavoko: Umepokelewa vizuri sana… sana maana ukiona umetoa wimbo baada ya siku mbili watu wanauimba ujue umekubalika sana.

Over Ze Weekend: Baada ya kujiondoa WCB, huoni kama unaweza kuwa umepoteza mashabiki wengi?

Mavoko: Kwa nini? Mimi ni yuleyule siku zote na mashabiki wangu hawabadiliki ni walewale tu.

 

Over Ze Weekend: Kwa sasa hivi kama mtu anakuhitaji kufanya shoo bado anakwenda WCB au tayari una mtu mwingine anayekusimamia?

Mavoko: Muziki bila kuwa na mtu anayekusimamia itakuwa ni shida, kama mtu ananihitaji anaonana na mimi kisha nitawaunganisha kwa watu wangu wa sasa.

 

Over Ze Weekend: Ni nani wanaokusimamia kwa sasa?

Mavoko: Hawapendi kuwekwa kwenye vyombo vya habari.

Over ze Weekend: Vipi WCB wakitaka kufanya shoo na wewe uko tayari?

Mavoko: Sina tatizo kabisa, tutakaa chini na kuzungumza si ni biashara tu?

 

Over Ze Weekend: Vipi tangu umejiengua, ulishawahi kwenda maskani yao kuwapa hi?

Mavoko: Unajua watu wanashindwa kuelewa, sikuondoka kwa ugomvi kule hata kidogo ni mambo tu ya kawaida ya kimuziki lakini sina tatizo na yeyote yule.

Over Ze Weekend: Nje ya muziki ni kitu gani kingine unachofanya?

Mavoko: Hakuna kitu kingine nafanya kwa sababu muziki ndiyo maisha yangu na ndiyo kila kitu kwangu.

 

Over Ze Weekend: Baada ya miaka mitano ijayo una ndoto za kuwa nani zaidi ya muziki?

Mavoko: Ndoto yangu kubwa ni kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki.

Over Ze Weekend: Vipi uhusiano wako wa kimapenzi na Lulu Diva umeishia wapi?

Mavoko: Hivi unajua sijawahi kusema au kukiri sehemu nina uhusiano na Lulu Diva! Nafikiri hayo ni mambo ya kazi na yameshapita.

 

Over Ze Weekend: Umeshaoa au una watoto? Maana wanamuziki wengi wanaogopa kuoa wanasema watashuka kimuziki?

Mavoko: Sijaoa bado ila nina watoto wawili, lakini kuoa ni jambo la kheri sana wanaosema wakioa watashuka kimuziki kwa hiyo wataoa lini sasa, uzeeni? Kwangu mimi muda ukifika nitafanya hivyo.

Over Ze Weekend: Shukurani sana kwa ushirikiano wako?

Mavoko: Asante sana!

Rommy Jones, Mlela, Hemedy walivyotoa Msaada

Comments are closed.