The House of Favourite Newspapers

Rich Mavoko Akinukisha BASATA, Sakata Lake na WCB – Video

MSANII wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amegeuka mbogo mbele ya waandishi wahabari baada ya kugoma kuzungumza kuhusu nini kinaendelea kwenye mazungumzo yake na uongozi wa Kampuni ya WCB ambako amekuwa akifanya kazi.

 

Mavoko amefanya kituko hicho jana wakati akitoka nje ya ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) alipokwenda kusuluhishwa na uongozi wa WCB kutokana na madai yake ya kwamba mkataba wake wa WCB ni wa kinyonyaji.

 

“Siwezi kuzungumza, kwani wewe nani, ninazungumza kwani unanilipa hela? Nilipe basi nizungumze…!” alisema Mavoko alihojiwa na wanahabari.

Aidha, alipotakiwa kuonyesha mwanasheria wake ili ahojiwa kuhusu mwenendo wa mashauriano hayo, Rich Mavoko alipanda kwenye ndinga na kusepa.

Kwa upande wa WCB iliwakilishwa na Meneja wake, Salam SK huku washauri ambao ni Basata wakiwakilishwa na Mtendaji wa Baraza hilo, Mungereza.

RICH MAVOKO Akinukisha/ Akosa Majibu Ishu Yake na Diamond

Comments are closed.