Rich Mavoko Asajiliwa Rasmi Lebo ya WCB

index

Msanii wa Bongo fleva, Rich Mavoko (kushoto)  akisaini Mkataba wa kujiunga na lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo chini ya staa wa tasnia hiyo, Diamond Platnumz (kulia).

index-001Diamond (kushoto) akipongezana na Rich Mavoko mara baada ya kusaini mkataba huo.

Habari ikufikie popote ulipo wewe mpenda burudani na mdau wa muziki wa bongo fleva kuwa, leo June 2, 2016 lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na staa wa tasnia hiyo Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi  msanii  wao mpya  Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika lebo ya WCB.

Kwa mujibu wa CEO wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz amesema…Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii nne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na jumla ya wasanii nne Raymond, Harmonize, Rich Mavoko na Queen Darling’Diamond Platnumz.3470
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment