The House of Favourite Newspapers

Rigwaride Ra Afande-13

0

ILIPOISHIA RISAJI JUMATANO:

“Usijali afande Mwira bwana. Kawaida sana, mimi nakushukuru kwa kila kitu, umenifaa maana nilikuwa sina kitu,” alijibu jamaa yangu. Akaja ndani. Lakini ghafla alisimama na kuniangalia sana…

SHUKA NAYO…

“Mbona macho yako mekundu na kama ulikuwa unalia?” aliniuliza…
“Ni kweli nilikuwa nalia…”
“Unalia nini?”

“Nawaza mama kunisusa hapa…”
“Hilo umelijua muda huu? Mbona muda wote ulichangamka?”
“Imetokea tu, hata mwenyewe nashindwa kuelewa.”
“Halafu mbona nasikia harufu ya jasho la mwanaume?”
“Mh!” Niliguna, nikaogopa mwenyewe…

“Mbona mimi silisikii,” nilisema nikijishauashaua na kuangalia pembeni.
“Niambie ukweli Rhoda, kuna mwanaume gani aliingia humu ndani?”
“Hakuna jamani! Kwani we umemuona nani?”

“Kuna harufu ya jasho la mwanaume humu, huwezi kunificha mimi,” afande alinijia juu. Na mimi niliendelea kukataa. Moyoni nilisema haitatokea nikakubali.
“Afande Mwira hajaingia?”

“Sijamwona. Na angeingiaje wakati nilikusikia ukisema unamshukuru kwa kukukopesha fedha. Si ina maana aliingia ndani kwake kukuchukulia!”
Niliposema hivyo tu, nilimwona afande Mwita akiishiwa nguvu na kukaa kwenye kochi…
“Wewe umejuaje kama alinikopesha fadha?” eti alitaka kubisha.

“Si nilikusikia hapa dirishani ukisema usijali afande Mwira bwana. Kawaida sana, mimi nakushukuru kwa kila kitu, umenifaa maana nilikuwa sina kitu.”
Afande Mwita aliishiwa nguvu. Akawa anaangalia pembeni huku akiimba nyimbo za kwao. Mimi moyoni nikasema ‘kwisha kazi wewe.’
***
Giza liliingia, sikumwona mama wala kupata simu yake. Nilikuwa nimelala wakati afande Mwira aliposema anakwenda baa kupata bia mbili tatu.
Nilipitiwa na usingizi na nilikuwa sijala, kuja kushtuka ni pale afande Mwira alipoingia chumbani akiwa amebeba mfuko wa rambo…

“Amka ule, nimekuletea chipsi kuku,” aliniambia.
Niliamka haraka sana. ilikuwa chipsi kuku mzima! Du! Mate yalijaa yenyewe mdomoni, akatoa na kopo mbili za bia. Nilijua pale tunazitumbua pesa za mkopo kutoka kwa afande Mwira…

“Kunywa na bia hizi,” alisema afande akiniwekea kwenye stuli…
“Asante baby…”
Kwa mara ya kwanza nilimuita baby lakini akanikataza nisimuite jina hilo yeye si mtoto…

“Nani baby wako wewe! Koma kabisa! Niite mpenzi. Mimi si mtoto mpaka unaniita baby.”
Nilijua jamaa zangu wa kule hawajuagi mambo hayo. Nikamwomba radhi na kumuita mpenzi.
Baada ya kula, tulikwenda kuoga wote. Taulo lilikuwa moja. Kwa hiyo nililivaa mimi, yeye akavaa bukta.

Tulipotoka kuoga tulipanda kitandani kulala. Kazi ikaanza hapo…
“Wewe mbona kama unasinzia. Hakuna kulala hapa,” aliniambia…
“Ha! We, yaani nisilale kisa nini wakati nasikia usingizi?”
“Hapa kwangu hakuna kulala.”

“Kwa nini? Ina maana na wewe hutalala?”
“Tutalala wote baadaye,” alisema na kuanza kunishikashika. Nikamwelewa sasa kumbe alikuwa na maana gani kusema kwake hakuna kulala…

“Sasa si ungesema tu,” nilisema moyoni huku nikianza kumuunga mkono kwa alichokuwa akikifanya yeye. Tulishikanashikana, tukashikanashikana.
Ni yeye ndiye aliyeanzisha mchezo na mimi nikaingia uwanjani kupambana naye.
Ilikuwa ni bandika bandua…bandika bandua!

“Sasa tungepumzika kwanza jamani,” nilisema…
“Tutapumzika,” alijibu kwa mkato huku akiendelea kupeleka mashambulizi upande wangu. Mwili uliisha nguvu lakini kama vile tena, sikuruhusiwa kutoka uwanjani kabla kipyenga cha mwisho wa mchezo hakijapulizwa.
Ilifika mahali mimi nikawa nalia tu kwa sauti ndogo maana sikuwa naweza hata kusogeza mpira hatua tatu mbele lakini nilimshangaa mwenzangu yeye, nguvu kama ndiyo kwanza anaanza mechi.

Shetani akamjalia akanitangazia kwamba anafika juu ya kichuguu, ikawa salama yangu. alipofika kichuguuni alijitupa huko, akajilaza akiangalia juu na kuhema kwa nguvu.
Tulipitiwa na usingizi bila kujijua, tukauchapa usingizi. Mimi nilikuja kushtuka saa tisa usiku baada ya kuangalia saa ya kwenye simu. Nilijisikia kwenda haja ndogo, nikamtingisha afande Mwita ili aamke, anisindikize…

“Nini wewe?” aliniuliza.
“Nisindikize chooni bwana.”
“Hapa kwetu hakuna wachawi, wezi wala vibaka, wewe nenda tu,” alisema afande Mwita huku akigeukia ukutani…

“Bwana mimi naogopa peke yangu.”
“Hivi husikii wewe. Unadhani nani atakuja kujibanza hapa kwa maafande, hajipendi?”
Nikatoka hadi chooni. Ile nageuza kurudi ndani, yule afande mbaba naye anatoka kwake, akanishika mkono…

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Risasi Jumatano ijayo.

Leave A Reply