The House of Favourite Newspapers

Rigwaride Ra Afande -8

0

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

Wakati anasema hivyo alikuwa akitembea kuelekea ndani, nikamfuata kwa nyuma mpaka ndani kwake, yaani chumbani kwake. Nilichobaini ni kwamba, ile nyumba kila mtu alikuwa ana chumba tu. Na chumba hicho ndiyo kilikuwa sebule na chumba cha kulala…

“Kaa hapo,” aliniambia akinionesha kochi kubwa. Nikakaa pwaa! Maana mimi naye, wowowo peke yake ni shughuli nzito…

TAMBAA NAYO MWENYEWE…

Nilijitupa kwenye kochi na kumwangalia yule mwanaume ambaye naye alionekana kunishangaa sana mimi lakini sikujua ni kwa nini anishangae vile…

“Kwani wewe una matatizo gani na mama yako mzazi?” aliniuliza yule mwanaume huku macho yake yakipepesa kwingine na si kwangu…

“Unajua mama ‘angu ana matatizo makubwa. Eti kisa nilikuwa humu ndiyo akamaindi na kuamua kunirudisha.”

“Ulikuwa humu kweli au ulimdanganya?”

“Nilikuwa humu kweli?”

“Humu kwangu?”

“Hapana, kwa afande Mwira.”

Niliamua kukomaa na afande mmoja tu kwa vile nikisema watatu, ningekuwa kituko cha mwaka huu unaoisha kwa tumbuatumbua.

“Ni nani yako?”

“Mpenzi wangu wa ghafla.”

“Khaa! Mpenzi wako wa ghafla? Oke! Sasa unadhani mpaka afande arudi usiku wa saa kumi utalala wapi?”

“Nitarudi nyumbani.”

“Mama ‘ako atakuelewa?”

“Najua hatanielewa,  lakini sasa wewe unadhani mimi nitalala wapi kama siyo nyumbani?”

“Oke..umekula?”

“Sijala na njaa imenikaba ile mbaya.”

“Nikupe nini ule?”

“Umepika nini kwani?”

“Sijapika chochote. Wewe sema utakula nini?” aliuliza huku akiniangalia kwa macho yenye maswali mengi kuhusu mimi.

“Utakachoamua wewe mimi nitakula tu,” nilimjibu kwa sauti iliyojaa ushawishi kwa mwanaume yeyote rijali wa kweli.

Alikwenda kwenye friji, akatoa mayai matano, akaenda pembeni ya mlango ambapo pana meza yenye jiko dogo la gesi, akasetiseti mambo yake pale, akaanza kukaanga mayai bwana.

Alipomaliza akayaleta meza ndogo ya katikati kisha akaenda kuchukua chupa ya chai, akaileta, akarudi tena kwenye friji akatoa mkate, akauleta mezani, akaniambia karibu chai…

“Nakunywa peke yangu?” nilimuuliza kwa sababu nilimwona yeye akikaa kwenye kochi jingine pembeni…

“Sasa ulitaka unywe na nani? Afande Mwira si nimekwambia atarudi usiku sana?” alisema.

Nilihisi anaweza kuwa mwanaume mwenye utofauti na wenzake. Hakuonekana kunishobokea kama maafande wenzake wa mwanzo, akina afande Mwira.

Nilijiungia chai, nikanywa wewee na mayai yote matano nikayamaliza, nikashiba vizuri sana. Nilitoa vyombo mwenyewe nikaviweka kwenye ndoo chini ya meza ya jiko. Nikarudi kukaa na kumshukuru huku simwangalii usoni…

“Nakushukuru sana kwa chai, nimeshiba,” nilisema, lakini hakujibu, nikamshukuru tena, pia hakujibu, nikamwangalia. Kumbe alikuwa amelala zamani gani!

Nilimfuata na kumtingisha…

“Oyaa! Anko…anko.”

Alishtuka na kunikodolea macho mekundu ya kutoka kulala…

“Vipi?” aliniuliza…

“Nasema asante sana kwa chakula. Nimeshiba.”

“Sawa, pumzika sasa, ukijisikia kwenda kwenu nenda,” alisema, akaendelea kujiliza.

Nilianza kuamini kuwa, duniani kuna wanaume wakamilifu na wengine siyo. Na huwezi kumjua kwa kumwangalia kwa macho ya kawaida mpaka vitendo.

Yaani jamaa alivyo na mvuto, mwili wenye siha njema, yuko na binti kama mimi, mbichi, nina mvuto wa kisichana halafu anachengachenga…mh!

Nilichofanya, badala ya kukaa pale kwenye kochi, nikaenda kujilaza kitandani. Miguu ilining’inia, kuanzia kiunoni kwenda juu kulikuwa kitandani.

Kila dakika kadhaa, niliinua shingo kumwangalia mwenyeji wangu pale alipolala, nikabaini anakoroma…

“Loo! Maskini…ananikosa hivihivi kwa kuendekeza usingizi,” nilisema moyoni huku na mimi nikiwa nanyemelewa na usingizi kwa mbali maana nilikuwa nalishia kama samaki kwenye bwawa.

Nilishindwa kujivumilia, maana mwanaume ni mwanaume, mwanamke ni mwanamke, kitendo cha kuwepo wawili chumbani kwangu hakikuvumilika. Afadhali basi angekuwa anko wangu au mtoto wa shangazi, lakini simjui, hanijui, loo!

Niliinuka, nikatembea kwa kunyata mpaka alipokuwa amelala, nikakaa jirani yake lakini nikijitahidi nisimguse kwanza.

Baada ya kukaa, nilimgeukia kumwangalia. Kumbe alikuwa ametoka kunyoa, nilikuwa nahisi manukato ya kunyolea yale.

Nilipeleka mkono kumshika kidevu, nikakipapasa, akatingishika, nikaacha. Akaendelea kukoroma, nikapeleka mkono kifuani, nikaanza kumpapasapapasa kwa mbali sana, akatingishika, akapeleka mkono pale kifuani kama aliyehisi pana mdudu kwa hiyo alitaka kumtoa. Nikaacha, akaendelea kukoroma.

Nikapeleka mkono kinywani sasa maana kinywa kilikuwa wazi, akakivuta na ulimi, nikakitoa. Nikajua kumbe anapenda vitu vikiwa kinywani, nikamsogelea huku natoa ulimi, akapanua kinywa tena!

Je, nini kiliedelea hapo? Usikose kusoma kweli Risasi Jumatano ijayo.

Leave A Reply