Rihanna Awatega Mashabiki Wake

rihanna-room-5Rihanna

DIVA wa muziki wa Pop, Rihanna ameendeleza kuwatega mashabiki wake kwa kushirikiana na Kampuni ya Sumsung baada ya kuachia vipande vingine vya video alivyoviita ANTIdiaRY ambapo ameachia chumba namba tano.

Katika chumba hicho cha tano, Rihanna anaoenekana akiwa ndani ya jakuzi akioga kisha anainamisha kichwa chini na kuinuka na baada ya hapo kupitia mlango wa vioo wa bafuni hapo anaonekana mtoto mwenye taji kichwani aliyetumika katika albamu mpya.

Rihanna aliamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwavuta karibu mashabiki wake wenye shauku ya kuipata aolbamu yake mpya na ya nane ijulikanayo kama ANTI.

VIDEO: RIHANNA NDANI YA ANTIDIARY CHUMBA NAMBA 5 

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Loading...

Toa comment