The House of Favourite Newspapers

Rihanna Amshtaki Baba Yake Mahakamani

 

MWIMBAJI nyota  Rihanna amemshtaki baba yake mzazi (Ronald), kwa kosa la kutumia chapa ya familia ya “Fenty” kinyume cha sheria kwa lengo la kujiingizia kipato kwa kufungua kampuni yake ya “Fenty Entertainment”.

 

Mtandao mmoja nchini Marekani umeripoti kuwa mwimbaji “Rihanna Fenty” amempeleka baba yake mahakamani akidai anatumia umaarufu wake kutengeneza kipato akiwa na mfanyabiashara mwenzake, Moses Perkins.

 

Mzee Fenty amekuwa akifanya kazi kama wakala wa Rihanna kinyume cha sheria, na tayari amepata shoo ya dola milioni 15 ambayo ni ziara  na matamasha mawili huko Amerika ya Kusini.  Shoo nyingine ni za Staples Center mjini Los Angeles, T-Mobile Arena mjini Las Vegas,  zote mbili akivuta mkwanja wa dola $400,000 (Sh. milioni 921)

 

Rihanna ameenda mbali zaidi na kutaka fidia kutoka kwa mshua wake huyo, pia ameitaka mahakama kusimamisha shughuli za kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2017.. Hata hivyo,  pamoja na yote hayo, Rihanna ametangaza kuja na nyimbo zake ambazo zitaingia sokoni hivi karibuni.

 

Comments are closed.