Ripoti Benki Kuu ya funga mwaka 2023; Sekta ya Maliasili Yapata Mafanikio
Ripoti mpya ya Benki Kuu ya funga mwaka 2023 katika sekta mbalimbali iliyotolewa Februari 16, 2024, inaonesha mafanikio ya kihistoria katika sekta mbalimbali hususani utalii kama ifuatavyo:
1. Kwa ujumla, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wakati wa Uviko mwaka 2022 juhudi za Rais Samia zimefanikisha kuongeza idadi ya watalii kwa takribani asilimia 100 kutoka watalii laki 922 mwaka huo hadi watalii milioni 1.808 mwaka 2023;
2. Kwa idadi hiyo pia ya watalii wa kigeni imevunja rekodi ya juu ya nchi iliyopata kufikiwa mwaka 2019 kabla ya Uviko ya watalii milioni 1.5 kwa kuivuka na sasa kwa Tanzania kufikisha watalii wa kigeni milioni 1.8 kwa mwaka kwa watalii wa nje ni rekodi mpya ambayo haijafikiwa tangu Uhuru. Idadi kamili ya watalii wa ndani itapatikana mwisho wa mwezi huu;
3. Si idadi ya watalii wa nje tu bali hata mapato, inaonesha ripoti hiyo, yamevunja rekodi kwa kuingiza Dola Bilioni 3.37 (takribani TZS Trilioni 8) mwaka 2023 kutoka Dola Bilioni 1.3 mwaka 2021 na Bilioni 2.3 mwaka 2022. Rekodi ya juu zaidi ya mapato kuwahi kufikiwa nchini katika sekta hiyo ni Dola Bilioni 2.6 mwaka 2019 kabla ya Uviko sasa imevunjwa na kuwekwa rekodi mpya.
Mwaka 2024 kazi zaidi inapaswa kuendelea kwa mipango na mikakati zaidi.