The House of Favourite Newspapers

Ripoti Maalum Ni kweli kuna dawa za kuongeza nguvu za Kiume – 4

0

NI wiki ya nne tukiendelea kuwaletea mada hii ambayo wataalamu mbalimbali wa afya ya binadamu wanatuelimisha kuhusiana na matatizo ya nguvu za kiume ambayo sasa ni kama janga kutokana na wengi kuathirika na maradhi hayo.

 

Mada hii imekuwa ikijadiliwa na madaktari watatu, Dk. Marise Richard, Dk, Godfrey Chale na Dk. Leopord Mwinuka ambao wana zahanati za kuwahudumia binadamu lakini pia Mtaalamu wa Lishe, Abdallah Mandai, leo atapata nafasi ya kuelimisha kuhusu jinsi ya kuondoa tatizo la nguvu za kiume kwa kutumia vyakula vya asili, endelea: Mandai anasema vyakula vya nafaka ambavyo vimesheheni nishati nyingi na zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari, husaidia kutunza uzito wa mwili pia husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu na huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kuongeza nguvu zake za kiume.

“Kula nafaka zisizokobolewa kama vile brown bread (mkate wa kahawia) uliotengenezwa kwa ngano isiyokobolewa badala ya white bread (mkate mweupe) pia kula nafaka halisi ni jambo zuri kiafya na kunafanya mwili kutopata mafuta mengi, ikumbukwe mafuta mengi kwenye damu yanaharibu mishipa ya damu ikiwamo ya uume. “Tangawizi ni aina ya kiungo mizizi ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Mzunguko unapokuwa mzuri huwezesha damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi ikiwamo uume.

 

“Tangawizi imekuwa ikitumika sana maeneo ya asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume,” anasema Mandai. Viungo ambavyo viko katika pilau huvaa kutumiwa na wenye matatizo ya nguvu za kiume kwani ni viungo vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume.

 

Akaongeza: “ Kuna matunda yanayoitwa komamanga, kitaalamu Pemigranate yenye rangi nyekundu husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumwongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.” Mvinyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu huku ikimwondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa. Hii ndiyo sababu kubwa kuikuta ikiwekwa vyumbani katika hoteli nyingi kubwa duniani. Nchi kama Italia mvinyo ni kinywaji ambacho hakikosekani mezani kutokana na kuaminika miaka kwa miaka kwamba inasaidia kuongeza nguvu za kiume.

 

Unywaji wa kiasi unaweza kuwa na faida kubwa kwa kuchochea na kuamsha hisia na kuweza kwenda mizunguko kadhaa. Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda ikiwamo tikiti maji, mbegu za maboga husaidia kuondoa acid mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.

 

KIUME Vanila husaidia kuamsha hamasa mwilini, vanila ni aina ya kirurubisho ambacho huwamo ndani ya vyakula ikiwamo ice cream. Asali ina madini yanayoitwa boron ambayo husaidia mwili kupata homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume. Hata vitabu vya dini hueleza ulaji wa asali na masega yake kama mlo wenye kuupa mwili nguvu. Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu na kuuimarisha mzunguko huo katika maeneo ya uzazi, hivyo kuongeza nguvu za kiume kwa mtumiaji mwanaume.

 

Pia karanga zina madini muhimu kama vile magineziamu, tindikali ya foliki na madini ya zinki ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume na kuongeza hisia. Vyakula vingine vinavyoongeza nguvu za kiume vikiliwa kwa utaratibu unaofaa ni pamoja na pilipili manga, mdalasini, makomamanga, kweme, njugu mawe nk. Baada ya kuona makala zilizoeleza sababu mbalimbali zinazosababisha matatizo ya nguvu za kiume, sasa tuwe pamoja kwa nguvu zote katika kipengele muhimu kinachohusu suluhisho la matatizo ya nguvu za kiume. Kikubwa unachotakiwa kufanya ili kuweza kupata msaada wa tatizo hili ni kuwa tayari kuweka wazi tatizo lako kwa watoa huduma za afya wa tiba za binadamu na siyo kwa watoa huduma wasiotambulika.

 

Ikumbukwe kuwa kuficha tatizo lako na kuendelea kusikiliza maneno ya vijiweni kwa marafiki ambao hawana uelewa na mambo haya kunazidi kukuchanganya na kukuchelewesha katika kupata matibabu sahihi, sehemu sahihi na kwa wakati muafaka. Wagonjwa wengi huwa na aibu kufika katika huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hilo wakihofia kunyanyapaliwa, lakini jambo hilo halipo kwa wataalamu wenye taaluma ya tiba za binadamu. Kumbuka kuwa si wewe pekee uliye na tatizo hilo, ni mamilioni ya watu duniani kote wana tatizo hilo hivyo unatakiwa kujiamini na kujipa moyo kuwa tatizo hili linatatulika.

 

Wengi hutumia dawa zisizothibitishwa jambo ambalo ni hatari. Unaweza ukawa unatumia dawa hizo na kupata nafuu na kudhani umepona, lakini kumbe ukawa unaudhuru mwili wako pasipo kujua. Dawa hizo zisizothibitishwa wala kupendekezwa kama ni salama na Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA), zipo kila mahali mitaani na wengi hujikuta wakinunua na kuzitumia kiholela. Miaka ya nyuma tatizo hili lilikuwa linaonekana kujitokeza zaidi kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea.

 

Lakini katika siku hizi hata vijana wa kati ya umri wa miaka 20 na 30 wanajikuta wanapatwa na tatizo hilo kutokana na wengi kutofanya mazoezi na kutozingatia vyakula vya kula. Tatizo la nguvu za kiume linaweza kutibiwa au likapunguzwa makali kwa matibabu mbalimbali baada ya kufanyiwa uchunguzi yakinifu. Dk. Marishe Richard anasema yapo matatizo ya nguvu ya kiume ambayo hujikuta hayatatuliki kwa njia yoyote, hivyo mtu mwenye tatizo hilo huwa ni ulemavu wa kudumu. Je, mitishamba hutibu ugonjwa huu?
Fuatilia wiki ijayo.

NA ELVAN STAMBULI

Leave A Reply