The House of Favourite Newspapers

Ripoti ya Bangala yatua TFF, adhabu iko hivi…

0

SHIRIKISHO la Soka Tanzania ‘TFF’ limesema limepokea ripoti ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Jumamosi iliyopita huku wadau wengi wakisubiri kuona mlinzi wa Yanga, Yanick Bangala atakutana na rungu gani.

 

Bangala alionekana akionyesha ishara isiyokuwa ya kiungwana dakika ya 59 ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Kupitia ripoti iliyokabidhiwa na mwamuzi Kayoko, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), inaweza kumtia hatiani Bangala kwa mujibu wa kanuni ya 39 ibara ya 5 ya udhibiti wa wachezaji ambapo anaweza kufungiwa michezo mitatu na faini isiyopungua Sh 500,000.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema: “Baada ya mchezo wa Jumamosi wa Simba dhidi ya Yanga, mwamuzi Ramadhani Kayoko aliwasilisha ripoti ya mchezo huo kwa kamati zinazohusika, na kupitia mwenendo wa mchezo kama kanuni inavyomtaka kufanya hivyo ndani ya saa 24.

 

“Hivyo kuhusu hilo tukio la mchezaji wa Yanga na changamoto zote za kinidhamu ambazo zilitokea kwenye mchezo huo, na baada ya kupitiwa ripoti hiyo tunatarajia kutoa taarifa ya maamuzi hivi karibuni.”

Joel Thomas, Dar es Salaam.

Leave A Reply