The House of Favourite Newspapers

Ripoti yabaini Rais kiir na Machar wanafaidika na vita

salvaRais Salva Kiir (kulia) na aliyekuwa makamu wake bwana Riek Machar 

Waziri wa habari Sudan Kusini amesema kuwa serikali haitajibu madai ya ripoti mpya inayodai kuwa viongozi wa nchi hiyo wananufaika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinayoendelea nchini humo.

salvaa

sehemu ya uharibifu wa vita hivyo.

Michael Maquei Lueth amesema kuwa serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu madai hayo lakini itafanya hivyo ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.

Ripoti iliyosimamiwa na muigizaji wa Hollywood na mwanakampeni George Clooney inadai kuwa Rais Salva Kiir, kiongozi wa upinzani Riek Machar na mkuu wa jeshi pamoja na familia zao wanafaida zinazofanana kulingana na vita baina yao.

Inawaunganisha wasomi wa Sudan Kusini katika mchezo wa fedha unaojumuisha nyumba za kifahari, migodi, mafuta na kampuni nyengine.

CREDIT: BBC.

 

Comments are closed.