The House of Favourite Newspapers

Riyama Aeleza Sababu za Kufutuka

Riyama Ally.

 

STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally ameeleza sababu zilizomfanya anenepeane baada ya watu kumponda kwamba, amekuwa na ‘minyama uzembe’ hadi kaharibika.

 

Akifungukia unene wake huo, Riyama aliliambia Risasi Jumamosi kuwa amelazimika kunenepeana kwa sababu sasa hivi anacheza nafasi ya umama kwenye filamu mbalimbali hivyo ameona ili kuuvaa uhusika vizuri, ajiachie ili awe na muonekano wa kimama.

 

“SIWEZI kupungua kwa sasa hata iweje, iwapo nitapata kazi inayo­taka nicheze nikiwa nimepungua basi nita­fanya hivyo, lakini kwa sasa nimelipwa kuwa hivi nilivyo,” alisema Riyama.

 

MAKALA: HAMIDA HASSAN

Comments are closed.