Riyama: Kipaji Changu Kilikuwa Kuimba Kuliko Kuigiza

Msanii wa filamu nchini Riyama Ally amesema kuwa ndoto yake kubwa wakati anakuwa alikuwa anapenda kuimba lakini mambo yakaja kubadilika hapo baadae na kujikuta anaingia kwenye uigizaji.

 

Mwanamama huyo ambaye alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuigiza kwenye filamu ya fungu la kukosa, ameendelea kueleza kwamba baada ya kuona kwamba yeye ndio anaupenda muziki lakini muziki haumpendi yeye ndipo alipoamua kugeuza gia na kujikuta akiwa msanii mzuri wa filamu.

 

“ Nilikuwa napenda sana kuimba, yaani popote utakaponikuta nilikuwa naimba nyimbo za Khadija Kopa, lakini mwisho wa siku nikaona kama najilazimisha kufanya hivyo maana hata kucheza nilikuwa siwezi, lakini kuna kipindi nikaja kukutana na watu ambao wakaniingiza kwenye filamu nikafanya poa na ndio mpaka leo naendelea kuzifanya,” alisema.

Stori: Memorise Richard

Toa comment