Riyama: Tusipopata mtoto, tutalea yatima!

STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally amesema bado ana matumaini ya kupata mtoto na mumewe Leo Mysterio na hata ikitokea hawajapata, basi watalea hata watoto yatima.

 

Akibadilishana mawazo na Amani, Riyama alisema waliingia kwenye ndoa mwaka 2016 kila mmoja akiwa na mtoto wake hivyo wanaamini Mungu atawapa mtoto wa kwenye ndoa yao na hata ikitokea wakakosa pia watamshukuru Mungu kwa kuwabariki watoto wawili wa kike kwani mumewe anaye mtoto wa kike na yeye anaye wa kike.

 

“Na iwapo tutataka kuongeza watoto tusipojaaliwa na Mwenyezi Mungu inshaallah tutawalea watoto wasiojiweza kwani nao ni watoto wetu,” alisema Riyama.

Stori: Mwandishi Wetu

Toa comment