The House of Favourite Newspapers

Riyama: Umbumbumbu umeniachisha shule

0

Riyama-Ali-532Staa wa Filamu Bongo, Riyama Ally

Na Brighton Masalu

KILAZA! Staa wa Filamu Bongo, Riyama Ally ameweka wazi kuwa hakumaliza elimu ya sekondari kutokana na ugumu wa masomo kwani hakuwa akiambulia chochote darasani licha ya walimu kujitahidi kufundisha kwa kiwango cha juu.

Riyama3Akizungumza na Ijumaa  hivi karibuni, Riyama alisema kuwa kutokana na umbumbumbu wake alilazimika kuishia kidato cha pili baada ya masomo kuzidi kuwa magumu.

“Kwa kweli ugumu wa masomo ulinifanya niache shule, niliona kama wazazi wanapoteza pesa yao bure, sikuwa naambulia chochote, walimu walikuwa wakijitahidi sana lakini sikuwa naelewa kitu, kwa hiyo nimekomea kidato cha pili, masomo magumu asikuambie mtu,” alisema Riyama.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWSglobalbreakingnews.JPG

 

No Comments
  1. […] Chanzo: GPL […]

Leave A Reply