The House of Favourite Newspapers

Robert Kearns aacha somo kubwa la utajiri duniani

0

Robert_KearnsRobert Kearns

KAMA wewe ni mfuatiliaji utagundua kuwa dunia imetawaliwa na watu wenye ubongo unaofanya kazi kwa haraka. Unapowaona mabilionea wa dunia kama Bill Gates, Carlos Slim na wengine, usishangae ni kwa nini wanaogelea kwenye utajiri ilihali wana ubongo kama wewe.

Bill Gates hana akili zaidi yako ila anachokifanya ni kuupa kazi ubongo wake, ufikirie zaidi ya wengine wanavyozipa kazi bongo zao kufikiria, hapo ndipo utofauti unapoonekana.

Ukiangalia ulimwengu wa sasa, huwezi kuwa tajiri bila kuwa mbunifu. Ili uwe tajiri ni lazima ubuni biashara ambazo zitakuwa na mvuto. Leo mtu akiwa anafanya biashara ya vitumbua sehemu fulani, ukitaka ufanye biashara kama yake eneo lilelile ni lazima uongeze vitu fulani katika vitumbua vyako ili kuleta tofauti.

Robert KearnsRobert Kearns na familia yake.

Ukitaka kufanikiwa zaidi, hebu angalia eneo ulilopo, kuna vitu vipo na vingine havipo kabisa. Kama kuna kitu hakipo na watu wanakihitaji, kwa nini usikipeleke kitu hicho mtaani kwako utengeneze fedha?

Watu wana shida ya maji mtaani kwako, kwa nini usipeleke tanki la maji uanze kuuza maji upate fedha? Watu wanauza chipsi mtaani kwako na unajua hawana mishikaki, firigisi au soseji, kwa nini usifungue biashara ya chipsi mahali hapo na kuongeza vitu ambavyo wao hawana?

Hakuna biashara mpya duniani, ila unachotakiwa kufanya ni kuongeza ubunifu katika biashara zilizopo ili utusue kama alivyotusua Robert Kearns.

ILIKUWAJE KWA KEARNS?

Huyu jamaa alizaliwa mwaka 1927 huko Indiana, Marekani. Alifariki dunia mwaka 2005. Jamaa alizaliwa katika familia maskini kama ulivyo wewe. Baada ya kuhangaika huku na kule kupata elimu, mwisho wa siku alijiunga na Chuo cha Detroit Mercy, alipoona hapo hakumtoshi alihamia kwenye Chuo cha Wayne State kisha akahamia tena katika Chuo cha Case Western Reseirve nchini Marekani ambako alitunukiwa digrii yake.

Kuna siku Kearns alikuwa akiendesha gari lake aina ya Ford. Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na hakuwa akiona vizuri mbele kutokana na maji yaliyokuwa yakimwagikia kwenye kioo. Alipofika nyumbani kwake, akatulia chumbani na kufikiria kuhusu hali aliyokutana nayo ndipo akapata wazo la kuanzisha kitu kiitwacho ‘wiper’ (kifaa kinachosafisha kioo).

Baada ya kupata wazo lake hilo, akawapelekea kampuni za magari za Ford na Chrysler akiwaambia lingekuwa jambo jema kama wangefunga kifaa hicho kwenye magari yao. Jamaa hao walikataa ila baada ya wiki chache, Kearns akashangaa kuona magari mapya ya Ford na Chrysler yakiwa na wiper katika vioo vya magari yao.

Hapo ndipo alipofungua kesi na baadaye kampuni hizo kutakiwa kumlipa.

Kampuni ya Ford ilimlipa dola milioni 10. 2 (zaidi ya Sh. bilioni 20) huku Chrysler ikitakiwa kumlipa dola milioni 18.7 (zaidi ya Sh. bilioni 40).

TUNAJIFUNZA NINI?

Unapokuwa na wazo au ubunifu fulani, usiishie kuufikiria na kuuacha tu. Ni lazima uufanyie kazi. Vuta picha kama Kearns aliyefariki dunia mwaka 2005 kwa ugonjwa wa kansa asingethubutu kutoa wazo lake, angezipata fedha hizo?

Profesor Jay “Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Magufuli Niliyoyaona ni Haya Hapa’

Leave A Reply