Robo Fainali Europa: Wolves vs Sevilla, Man U vs Copenhagen

LIGI ya Europa imeendelea jana katika hatua ya mtoano ya 16 bora ambapo timu za Sevilla, Basel, Bayer Leverkusen na Wolves ziliibuka na ushindi na kutinga hatua ya robo fainali.
Timu hizo zimeungana na FC Copenhagen, Shakhtar Donetsk, Inter Milan na Manchester United zilizoibuka na ushindi juzi na kutinga hatua ya robo fainali.
Katika hatua ya robo fainali, Inter Milan itavaana na Bayer Leverkusen huku Manchester United ikikutana na FC Copenhagen mnamo Agosti 10, 2020.
Aidha, mtanange kati ya Wolves na Sevilla na ule wa kati ya Shakhtar Donetsk na Basel utakuwa Agosti 11, 2020. Michezo yote kuanzia hatua hii itapigwa nchini Ujerumani.


