#GlobalMusic: Rock City Rapa COYO Amerudi Na Nyingine Mpya ‘ZIWAFIKIE’ – (Official Music Video)

Kwa wale wadau wote wa Hip Hop na wenye mapenzi ya dhati na Mwanza, ipokee nyingine mpya kutoka kwa Tetemesha Entertainment na Coyo.

Baada ya kuachia wimbo wake wa kwanza ‘Njoo Baadae’ mwishoni mwa mwaka jana, COYO rappa kutoka Rock City Mwanza anatukutanisha na video yake mpya ‘ZIWAFIKIE’, iliyosimamiwa  na mmoja ya music directors wakubwa kutoka Arusha, Nisher.

Akizungumzia video yake mpya na sababu za kufanya kazi na Nisher Coyo amesema:

Naweza kusema hii ndio video yangu ya kwanza ramsi, japo nimewahi kufanya video zingine hapo kabla ambazo nahesabu kama ilikuwa ni safari ya kujifunza… Sababu za kumchagua Nisher, kwanza kiukweli nazikubali kazi zake, nalikubali jicho lake na kwa kuzingatia hii ndio video yangu rasmi ya kwanza, nilihitaji kufanya na mtu makini kama yeye. ” –  Coyo.

Audio ya ‘ZIWAFIKIE’ ambayo inatarajiwa kuanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya radio baadae wiki hii au wiki ijayo. Wimbo umetayarishwa na maproducer wawili, Daydream na Kid Bway.

COYO – ‘ZIWAFIKIE‘ (Official Music Video).

Producers/ KidBway & Daydream.

Video Director/ Nisher.

Dressed By (Stylist)/ Mickyson (Mr.Outfit).

(C) 2017 Tetemesha Entertainment.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment