Roll Royce ya Diamond Alichagua Zari

GARI hilo aina ya Roll Royce Cullinan 2021 lenye rangi ya buluu linakadiriwa kuwa na thamani isiyopungukia shilingi milioni hamsini.
Muhtasari.

 

Akitangaza mafanikio hayo kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumatano, staa huyo alionyesha video akiwa amekalia gari lake mpya aina ya Roll Royce Cullinan 2021. Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo aina ya Bongo Flava, Diamond Platinumz ameongeza gari jipya kwenye gereji yake.

 

“Nimepokea Rolls Royce Cullinan 2021 yenye haijasafiri hata kilomita moja leo. Ni siku yenye baraka aje leo,” Diamond aliandika.

 

Kwenye video ambayo Diamond alipakia, magari mengine sita makubwa yalionekana. Gari hilo lenye rangi ya buluu linakadiriwa kuwa na thamani isiyopungukia milioni hamsini. Wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri walijumuika kumpongeza Diamond kwa kufanikiwa kununua gari la ndoto zake.

 

Ujumbe ambao ulisisimua wanamitandao wengi ni wa aliyekuwa mpenzi wake Zari Hassan. Ujumbe wa Zari ulifichua kuwa alimpatia ushauri kuhusu rangi ya gari hilo. “Nafurahi kuwa ulichagua rangi ambayo tulikubaliana. Hongera,” Zari alisema.

 


Toa comment