The House of Favourite Newspapers

ROMA, MAN FONGO ‘KUUMIZANA’ DAR LIVE JUMAPILI – PICHAZ

WASANII wa muziki wa Hip hop, Roma Mkatoliki na mkali wa Singeli, Man Fongo,  leo wamethibitisha kushiriki katika Tamasha la Shukrani ambalo lengo lake ni kuwashukuru wasomaji wa magazeti ya Global Publishers linalotarajiwa kufanyika Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

 

Wakizungumza na wanahabari, wasanii hao kila mmoja alitamba kufanya makamuzi ya aina yake ambapo Man Fongo aliahidi kuja na kundi lake akiwemo Dulla Migoma.

Roma naye aliahidi kuja na kundi lake ili kuinogesha shoo hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake na haitakuwa na kiingilio, yaani bure,  kuanzia saa 8:00 hadi saa 12:00 jioni na baadaye usiku patashuhudiwa game ya fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Croatia.

Wasanii hao wamethibitisha hilo kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika ofisi za Global zilizopo Sinza-Mori jijini Dar.

Akizunguma wakati wa mkutano huo, Meneja Mkuu wa Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, amesema siku ya tamasha hilo watatoa pia zawadi za pikipiki mbili kwa washindi wawili wa Shindano la Tusua Maisha na Global, washindi wa dinner set, headphones za beats by dre na jezi za Kombe la Dunia.

Mshiriki anatakiwa kununua gazeti lolote la Global Pulishers yaani; #Uwazi, #Amani, #Ijumaa,  #IjumaaWikienda,  #RisasiMchanganyiko,  #RisasiJumamosi,  #Championi, #SpotiXtra kisha kufuata maelekezo yaliyopo kwenye kuponi maalum ukurasa wa pili.

Maelezo kwa mshiriki ni: Nenda sehemu ya kutuma ujumbe (SMS), kwenye simu yako, andika namba  zilizopo kwenye kuponi ukurasa wa pili wa gazeti husika, kisha utatuma namba hizo kwenda namba 0719 386 533. (Hakikisha una salio au bando la kutuma meseji kwa kiwango cha kawaida tu).

Kisha jaza taarifa zako binafsi kwenye kuponi hiyo na tunza nakala ya gazeti lako kwani litahitajika wakati wa kuchukua zawadi yako. Kwa kutuma ujumbe, moja kwa moja unakuwa umengia kwenye kinyang’anyiro cha kujishindia  zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine zitakazotolewa kila wiki.

Namba yako itaingizwa kwenye droo itakayochezeshwa kila Jumamosi na kuonyeshwa moja kwa moja mtandaoni na Global TV Online. Utapigiwa simu iwapo utafanikiwa kujishindia zawadi yoyote kwa wiki husika. Kwenye gazeti kutakuwa na kuponi yenye taarifa zifuatazo; Jina kamili, namba ya simu, umri na mahali unapoishi.

 

Aidha, baada ya tamasha hilo, usiku kutakuwa na mechi ya Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Ufaransa na Croatia ambayo itaonyeshwa LIVE na kutakuwa na chakula pamoja na vinywaji.

Comments are closed.