ROMA: UKINICHANJA DAMU YANGU NI LOWASSA MTUPU

KWA sasa, ulimwengu wa burudani umetekwa na Ibrahim Musa ‘R.O.M.A’ baada ya kuchafua hali ya hewa na songi la Zimbabwe. Kabla halijapoa, mkali huyo amefanya fujo nyingine baab’kubwa kupitia ‘joint’ yao waliyoiita Rostam.
Katika ‘project’ ya Rostam ambayo R.O.M.A ameiunda kwa kushirikiana na mkali wa michano, Bonavetura Kibogo ‘Stamina’, imegeuka gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wimbo huo umeonekana kutazamwa na zaidi ya watu 53, 000 ndani ya muda mfupi katika mtandao wa YouTube.
Rostam (Roma & Stamina) – Hivi ama vile [Official Music Video]
Amani limezungumza na R.O.M.A juu ya ‘vurugu’ hiyo aliyoifanya muda mfupi ikiwemo kumuuliza sababu hasa za kuachia ngoma hizo kwa mpigo. Pia, Roma amefunguka mambo mengi yahusuyo muziki na maisha katika makala haya:
Amani: Joint yako na Stamina imekujaje haraka wakati Zimbabwe bado ilikuwa haijapoa?
R.O.M.A: Zilikuwa zitoke zote kwa nyakati moja na ilipaswa itangulie ya Rostam coz ni project ya album kabisa.
Amani: Rostam imetoka au itatoka lini?
R.O.M.A: Bado haijatoka na huo ndio wimbo wetu (Hivi ama Vile) wa kwanza kama utambulisho wa album.
Amani: Ooooh sasa huoni kama itaitoa haraka Zimbabwe sokoni sababu ilikuwa bado inahitaji muda wa kuendelea kupigwa?
R.O.M.A: Hilo sihofii kwa sababu, kama Zimbabwe ni mbaya itatolewa yenyewe sokoni lakini kama ni nzuri, zitaenda zote tu kwa mashabiki kila moja kwa nafasi yake. Ni vitu viwili tofauti. Zimbabwe ni R.O.M.A na hii nyingine ni ya wapinzani wa jadi, Stamina na R.O.M.A. Ni sawa na niwe na kolabo na mtu sasa hivi halafu nimzuie asiitoe kwa sababu atamtoa Zimbabwe sokoni.
Amani: Umesomeka, project ya hiyo albamu yenu ina ngoma ngapi na mtatoa albamu lini?
R.O.M.A: Ngoma nane tu ila tunafikiria kuongeza. Itatoka kabla mwaka huu kuisha. Amani: Kwa nini ni R.O.M.A na Stamina, isiwe R.O.M.A na msanii nwingine?

R.O.M.A: Aaaah ingekuwa na msanii mwingine pia usikute wangeuliza kwa nini ni R.O.M.A na msanii mwingine isiwe na Stamina! Vingine hutokeaga tu Mungu anapanga! Lakini pia nampenda mdogo wangu (Stamina) na nafurahi nikiwa nafanya naye kazi.
Amani: Vizuri mzee baba, lakini katika hii ngoma ndio tuseme umeamua rasmi kujidhihirisha kwamba wewe ni mfuasi wa Chadema na Edward Lowassa kwa ujumla sababu umesikika ukisema ukichanjwa damu yako ni Lowassa mtupu?
R.O.M.A: It’s just an art, ni sanaa tu kama vile joti akivaa nguo za kike halafu tumwambie amedhihirisha yeye ni demu! Ni sawa na Ferooz alivoimba Starehe amepata H.I.V tumhukumu kuwa ni muathirika kweli…?, no hii ni sanaa tu. Mi nimewaza, labda coz ngoma ilikuwa ni kubishana tu, model vs model, mwanasiasa kwa mwanasiasa, mchezaji mkubwa na mwenzake, na vitu kama hivyo, but nothing’s serious!
Amani: Kuna taarifa kwamba Nay wa Mitego hakufurahishwa na mstari wako uliosema ana kithethe katika ngoma hiyo, unamwambia nini wewe maana inaonekana ni bifu sasa hili ndugu msanii?
R.O.M.A: Niko naye hapa kila akisikiliza anacheka sana he is my friend so hakumaindi. Amani: Nini kinafuata baada ya Zimbabwe?

R.O.M.A: Nadhani kwa sasa ni ‘tudeal’ na Zimbabwe tu kinachofuata kikitaka kuanza nitawaambia… sasa hivi macho yote yawe Zimbabwe.
Amani: Ulimtanguliza mkeo, mama Ivan kutambulisha Zimbabwe, una mpango wa kumfanya kuwa meneja wako siku za usoni?
R.O.M.A: No la hasha! ‘Ame-play’ tu part ya kutambulisha wimbo basi.
Amani: Mama Ivan ameshawahi kukupa mchango katika vesi yoyote?
R.O.MA: No sema anaweza akasema futa hiki usiweke hiki japo yeye hawezi kuwa na cha kuweka ila cha kutoa anaweza kukiona.
Amani: Una mpango wa kolabo ya msanii kutoka nje?
R.O.M.A: Ndio hakika kabisa na hata hao wa nje wanataka kazi na mimi.
Amani: Kwa mfano nani wewe una-wish kuchana nae katika mdundo mmoja halafu na wewe ni nani ambaye anakuhitaji?
R.O.M.A: Eminem may be, kichaa wangu. Amani: Nilijua tu, sasa kwa upande wa Afrika ni nani unamkubali.
R.O.M.A: Kuna underground anaitwa Akadodi yupo apo mjini Uganda, namuelewa mno. Amani: By the way tangu lipite lile tukio baya la kutekwa, hujawahi kupata vitisho vyovyote au kupata hofu siku moja labda ukapaniki hivi?
R.O.M.A: Naamini katika Mungu so hofu ni dhambi.
Amani: Umejifunza nini kupitia tukio lile kutoka kwa mashabiki wako?
R.O.M.A: Nimejifunza vingi ila kubwa ni kuwa nina impact kubwa sana!
NA: ERICK EVARIST| AMANI


Comments are closed.