Roma Yamuibukia Beki wa Liverpool

SENTAHAFU wa Liverpool, Dejan Lovren inasemekana yupo njia moja kujiunga na Roma ya Italia. Roma inadaiwa imetenga kitita cha pauni milioni 15 (Sh. bilioni 42) ili kumsajili beki huyo wa Croatia. Mapema Roma iliwasiliana na Liverpool kuhusu uwezekano wa kumchukua Lovren kwa mkopo.

 

Liverpool iligomea mpango huo na kushikilia kuwa ilikuwa inataka kumuuza beki huyo. Gazeti la Corriere dello Sport la Italia limesema kuwa Roma imeamua kurudi kwa Lovren baada ya kukwama kumpata Daniele Rugani wa Juventus.

 

Roma inaaminika bado imeweka mkazo kwenye dili la mkopo ingawa sasa ina kazi ya kuishawishi Liverpool. Lovren hana namba katika kikosi cha kwanza cha Liverpool kutokana na kudhibitiwa kwa nafasi ya mabeki wa kati na Virgil van Dijk, Joe Gomez na Joel Matip.


Loading...

Toa comment