Kartra

Ronaldo Abeba Kiatu cha Dhahabu Euro 2020

Cristiano Ronaldo ametwaa kiatu cha dhahabu cha mashindano ya Euro 2020 baada ya kuibuka mfungaji bora wa mashindano.
✍️ Takwimu za Ronaldo:
🏟️ Mechi: 4
⚽ Magoli: 5
🅰️ Assists: 1
✍️ Cristiano Ronaldo anachukua kiatu mbele ya Patrick Schick wa Czech Republic baada ya kuhusika na magoli mengi zaidi ambapo ana Assist moja huku Patrick Schick akiwa na magoli matano na hana Assists hata moja na amecheza mechi 5.
✍️ Cristiano Ronaldo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya mpira wa miguu, kuwa mfungaji bora kwenye Champions league, Premier league, La Liga, Serie A na Euro.
Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Italia, Gianluigi Donnaruma amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2020.
Donnaruma anaweka rekodi ya kuwa golikipa wa kwanza kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Euro.
Taarifa nyingine kuhusu Donnaruma ni kwamba msimu ujao atakuwa kipa wa Klabu ya PSG.


Toa comment