RONALDO AFICHUA ATAPOSTAAFIA

Cristiano Ronaldo

STRAIKA wa Juventus, Cristiano Ronaldo amefi chua kuwa atamalizia soka lake nchini Ureno baada ya kumalizana na klabu yake ya sasa. Ronaldo, ambaye alijiunga na Juventus msimu huu akitokea Real Madrid, mkataba wake unatazamiwa kumalizika mwaka 2022.

Staa huyo wa timu ya taifa ya Ureno alidokeza anafi kiria nyayo za Nani kwa kumalizia soka yake kwenye timu aliyoanzia ya Sporting Lisbon.

“Ninafikiria kufuata nyayo za Nani kwa kurudi kwenye klabu niliyoanzia soka ya Sporting Lisbon,” alieleza Ronaldo. Aliongeza, hata hivyo, kwa sasa anafurahia maisha nchini Italia kutokana na mapokezi mazuri ya mashabiki wa Juventus.

Ronald o anaongoza kwa kufunga kwenye Serie A akiwa na mabao14 katika mechi 18. Pia staa huyo wa zamani wa Manchester United ametoa asisti tano kwenye mechi za Serie A.

Italia

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment