The House of Favourite Newspapers

Ronaldo Afikisha Wafuasi Milioni 500 kwenye Mtandao wa Instagram

0

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo @cristiano amekuwa mtu wa kwanza kufikisha wafuasi Milioni 500 kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

 

Naye nyota wa Klabu ya Paris Saint Germain na Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi @leomessi anashikilia nafasi ya pili akiwa na jumla ya wafuasi Milioni 375.64.

Nyota wa Paris Saint Germain na Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi

Katika nafasi ya tatu ni Mrembo na Mwanamitindo kutoka familia ya Kim Kardashian Kylie Jenner @kyliejenner.

 

Kwa sasa nyota huyo yupo katika mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia yanayofanyika nchini Qatar akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa ya Ureno ambapo mchezo wake wa kwanza atacheza dhidi ya Timu ya Taifa ya Ghana mnamo Novemba 24.

Leave A Reply