Ronaldo Avamiwa Na Mashabiki Akitoka Tizi

CRISTIANO Ronaldo juzi alionekana kwenye mazoezi ya timu yake ya Man United kwa mara ya kwanza huku akivamiwa na mashabiki waliolizingira gari lake la kifahari aina ya Lamborghini 4/4 wakati akitoka mazoezini, waliomshangilia na wengine wakinyanyua mabango ya kuonyesha kufurahishwa na ujio wake klabuni hapo.

Ronaldo, 36, ambaye alikuwa na gari lake aina Lamborghini 4/4 yenye thamani ya pauni 160,000, alionekana akiwa makini sana wakati anatoka na kuingia kwenye mazoezi hayo.

 

Mashabiki ambao walikuwa nje ya geti hilo walisikika wakimwambia tunafurahi kukuona tena umerudi hapa.

 

Hata hivyo, sasa mashabiki wa United wajiandae kuona magari makali aina ya Ferrari Monza, Rolls Royce, Mercedes G-Wagon na Bugattis ambayo yanamilikiwa na Ronaldo yakiingia mazoezini hapo.


Toa comment