The House of Favourite Newspapers

Cristiano Ronaldo na Mendes Wafanya Mazungumzo na Bayern Munich

0
Nyota wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo

NYOTA wa Manchester United, Cristiano Ronaldo huenda akajiunga na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani baada ya wakala wake Jorge Mendes kufanya mazungumzo na klabu hiyo.

 

Ronaldo (37) amekuwa katika mgogoro mzito na klabu yake ya sasa kutokana na kupigwa benchi na kocha wake Erik Ten Haag, na hivi karibuni ameibuka na kusema kuwa hamheshimu kocha huyo.

Wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes

Nyota huyo kwa sasa amejiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kinachojiandaa na mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwezi Novemba mwaka huu.

 

Nyota huyo ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora duniani Ballo D Or mara tano amekuwa akihusishwa pia na mpango wa kujiunga na miamba ya soka nchini Uingereza klabu ya Chelsea.

Leave A Reply