testiingg
The House of Favourite Newspapers

Ronaldo: Uhusiano Wangu na Bruno Fernandes ni Mzuri, Hakuna Shida

0
Nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo yupo tayari kuwakabili Ghana katika mchezo wao wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Qatar 2022

NYOTA wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amesema kuwa hana tatizo lolote na mchezaji mwenzake Bruno Fernandes na amesema uhusiano wao ni mzuri.

 

Vyombo vya Habari barani Ulaya vilichapisha moja ya video iliyoonesha nyota hao wakisalimiana katika taswira ambayo ilionesha kama hawako sawa kiuuhusiano na hiyo ilidhaniwa kuwa ni kutokana na mahojiano ambayo Ronaldo aliyafanya na mwandishi wa Habari Piers Morgan.

 

“Uhusiano wangu na yeye ni mzuri, nilikuwa namtania. Ndege yake ilichelewa kufika nikamuuliza endapo alikuja na Boti. Hivyo tu.” alisema Ronaldo.

 

Ronaldo kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kinachojiandaa na mchezo wa kwanza wa mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar dhidi ya Timu ya Taifa ya Ghana.

Leave A Reply