The House of Favourite Newspapers

Rooney: United Itatwaa Ubingwa EPL

0

 

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amesema anategemea Mashetani Wekundu (Manchester United) watatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

 

 

United ambayo mara ya mwisho kutwaa taji la EPL ilikuwa ni mwaka 2013 msimu uliokuwa wa mwisho kwa aliyekuwa Kocha wao, Sir Alex Ferguson, imeonekana kuimarika baada ya wiki iliyopita kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuifunga Fulham bao 2-1.

 

 

Akizungumzia matarajio yake, Rooney ambaye hivi karibuni alistaafu soka, amesema Ole Gunnar Solksjear amefanya kazi ya kushangaza na mambo yamebadilika ghafla, huku akipongeza usajili wa Bruno Fernandes na Edinson Cavani akiamini umeongeza chachu ya kushinda ubingwa kikosini.

 

 

Rooney ambaye ni mshindi mara tano wa EPL alipokuwa na Man United, amewataja Cavani na Fernandes kuwa ni wachezaji wenye kiu ya ushindi, na sasa wamemsaidia Paul Pogba kucheza akiwa huru na kung’ara, kitu ambacho kilikosekana kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha United.

 

 

Manchester United inaongoza ligi ikiwa na alama 40, ikifukuzana na Manchester City wenye alama 34 huku Liverpool ambao ndio mabingwa watetezi wakiendelea kuporomoka hadi nafasi ya tano wakisalia na alama 34.

Leave A Reply